Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya
kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania
milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na
Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo
ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya
kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania
milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo
kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara
baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za
Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje
Balozi Dkt. Aziz Mlima.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya
kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya
aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani
Kagera.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na
jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea
msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU
Hao waliofariki katika mtetemeko wa Kagere Mungu awarehem
ReplyDeleteNa walionusurika Mungu azidi kuwasaidia
Katika siku zilizopita nimekuwa nasoma kila siku hapa kwa Ankal misaada ya mali na vifaa vingine kutoka mbali mbali kuwasaidia jamaa hao. Iliyobaki sasa ni utengenezaji wa bodi maalum itakayokuwa na madaraka ya matumizi ya fedha hizo katika ujenzi wa maisha mapya ya ndugu zetu hao.Itasikitisha baada ya miaka tukisikia kuwa kulikuwa ba wajanja ambao kazi yao ilikuwa ni udokoaji na wizi kwa manufaa binafsi.