KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea na utekelezaji wa kuboresha
miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani, mkononi pamoja na huduma
za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wake na kufikia
kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini. Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na
wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa
maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa katika shirika hilo
yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali na kuwapa
wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa
kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa.
"Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa
miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za
Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia
kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema
Waziri Kindamba.
Aidha
alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba
itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika
kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko
watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii,
uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na
mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya
kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani
ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya
Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki,ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Thomas
Mushi (wa pili kulia) akipata picha na baadhi ya wageni waalikwa kwenye
hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika
ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja
vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili
kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...