Mwashungi
Tahir na Fatma Makame/Maelezo Zanzibar
Waziri
wan
chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema
uchumi wa Zanzibar unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia
saba na mfumuko
wa bei bado upo kwenye tarakimu moja na pato la Taifa linazidi kukua.
Ametoa
maelezo hayo ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama
cha mapinduzi Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali
Mohammed Shein.
Amesema
katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na ishara
zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura nzuri za
mafanikio.
Akizungumzia
suala la Muungano amesema unaendelea
kuimarika na vikao mbali mbali vya watendaji wakuu wa pande mbili
wakiwemo mawaziri vimeshafanyika na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ameshafanya vikao viwili vya kisekta kwa nia ya kutatua
changamoto zilizopo.
Waziri Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imekamilisha kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji
chapa na mpigaji chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.
Aidha
amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili
kuimudu teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi na
kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.
Sambamba na
hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya kuratibu na
udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa ya kulevya kwa
jamii.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa
tarifa ya mafanikio ya Ofisi yake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya chama
cha Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein Ofisini kwake Vuga
Mjini Zanzibar.
Wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa
akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake Ofisini kwake Vuga.Picha na
Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...