Bibi Josephine
Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto
Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa
hapo awali. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na
kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira
Mmiliki wa
Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri
Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua.
TAARIFA
YA ZIARA YA MHE. JANUARY MAKAMBA KATIKA MKOA WA KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe January Makamba hii leo ameendelea na
ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo
aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda
ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha
katika Mto Katuma.
Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara
yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa
Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
1. Ongezeko
la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.
2. Kusitisha
uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya
mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
3. Uchimbaji
hatari wa Madini usiofuata taratibu
4. Kuhuisha
sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
5. Kuanisha
maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira
nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi
6. Kusimamia
uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji
7. Kufanyika
kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora
ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira
8. ameahidi
kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma
9. Mmiliki
wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini
isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa
shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
10. Waziri
Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini
bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini
Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba
alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:
1. Wananchi
kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na
Uchomaji wa misitu.
2. kuwakumbusha
wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu
wachache
3. Serikali
inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo
ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998
4. Kuundwa
kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya
shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji
5. Kuundwa
kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho
6. Kuondokana
na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa
Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha
chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa
Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa
kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...