WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Jordan
Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Bw
Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi badala
ya karakana ya Magereza kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Magereza
mkoa wa Dodoma ilipewa sh. milioni 24 na Serikali ili kutengeneza
madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu sh. 50,000. Uongozi wa
gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi ambapo dawa moja
limegharimu sh. 70,000.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati
alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma Oktoba
5, 2016.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati
alipotembelea Gereza la Isanga mkoani Dodoma akiwa kwenye ziara ya
kukagua maeneo yanayotoa huduma za jamii mjini hapa.
Amesema
kama gereza hilo halikuwa na uwezo wa kutengeneza madawati hayo kwa
nini kazi hiyo wasingeipeleka kwenye taasisi nyingine ya umma, hivyo
amemtaka Mkuu wa Mkoa Bw. Rugimbana kufuatilia ziada ya sh. 20,000
kwenye utengenezaji wa kila dawati inatoka wapi na inakwenda kwa nani.
“Nimesikia
kwamba mnawachangisha askari kiasi kilichoongezeka kwenye utengenezaji
wa madawati hayo. Ni marufuku askari kutoa fedha mifukoni mwao kulipia
shughuli za Serikali,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mofisa na Askari Magereza baada ya
kutembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma Oktoba
5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augustine Mrema.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...