Halmashauri
tatu za Mkoa wa Mara zimevuka Lengo la Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now –
BRN) la asilimia 80 katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2016.
Hayo
yamesemwa leo, Wilayani Tarime na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mara Mwalimu Hamis Lissu alipokuwa akifungua semina ya
Mawasiliano na kushirikishana jitihada zenye mafanikio kwenye Elimu kwa maafisa
wa Elimu wa Mkoa wa huo.
“Halmashauri
za Tarime Mji, Tarime Manispaa na Musoma Manispaa ni halmashauri ambazo
zimevuka lengo la BRN katika Mkoa wa Mara, Halmashauri hizo kila moja zimepata wastani
wa asilimia 82 katika matokeo ya darasa la Saba ya mwaka, 2016,” alifafanua Lissu.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, ufaulu wa darasa la saba katika Mkoa wa Mara umekuwa ukipanda
mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka 2014, ambapo kwa mwaka 2014 Mkoa wa Mara ulikuwa
Mkoa wa 25 kati ya Mikoa 25, mwaka 2015 Mkoa ulishika nafasi ya 17 kati ya
Mikoa 25 na mwaka huu 2016 umeshika nafasi ya 13 kati ya Mikoa 26.
Lissu
amesema kuwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mara zimeongeza ufaulu katika matokeo
ya mwaka huu ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 na 2014.Vile
vile amesema kuwa ongezeko hilo la ufaulu limefanikishwa kwa kiwango kikubwa na
Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality Improvement
Programme -Tanzania) EQUIP-T unaosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kushirikiana na Serikali ya Uingereza.
Mpango
huo umekuwa ukitoa mafunzo ya kuboresha utendaji wa walimu darasani pamoja na
kutoa pikipiki kwa waratibu elimu kata wote ambao ndio wafuatiliaji wakubwa wa
ufundishaji wa walimu na maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi katika ngazi ya
kata.
Aidha
Lissu amesema kuwa kuna asilimia kubwa ya Mkoa huo kushika nafasi ya kumi bora
kitaifa katika matokeo ya mwaka 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...