Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili na kurejea nyumbani mara baada
ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa
hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais
mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya
kupata nafuu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani mara baada ya kupata nafuu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara
ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea
nyumbani baada ya kupata nafuu.
Picha na IKULU
Pole sana Mama Janeth MAGUFULI. Mola atakuafu pia kukujaaliya nafuu na kupona haraka. In Sha Allah.
ReplyDelete