Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Matokeo na wachezaji wenzie,katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (kushoto) na katibu mkuu wizara ya ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Mh Job Masima katikati katika mashindano ya Waitara Trophy Jumamosi Novemba 19
jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Mawazo na wachezaji mwenzi ambaye
ni katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (katikati) katika mashindano
yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu Wizara ya ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima.
Mshindi wa Jumla wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Juma
likuli akiwa amenyenyua vikombe alivyokabidhiwa na Jaji Mkuu Mh Othman Chande aliyekuwa mgeni
rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwa ameshika zawadi ya kikombe
alichokabidhiwa na Chama cha Golf Tanzania TGU ikiwa ni ishara ya Kutambua Mchango wa Klabu hiyo
katika kukuza mchezo wa Golf Nchini kulia ni mweka hazina wa TGU Akhil Yusuphali mara baada ya
mashindano ya Waitara yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...