Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,MIKUMI .
Mamlaka
ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi
inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha
watanzania tamaduni ,mila na desturi kuulinda utamaduni wetu , ambao
unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania .
Amesema utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema
chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Community College
cha nchini Canada kinaandaa kozi hiyo itakayowezesha watanzania
kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya
asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali.
Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
Aidha mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala.
Ayo amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa
rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro
kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa
sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na
serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka
msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda.
Mwalimu wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiendelea na mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi.
Mwalimu wa Chuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.
A very good move. Utalii wa kiutamaduni, utasaidia kuzalisha maelfu ya ajira kwa vijana
ReplyDeleteProfessionalism in tour guiding is important, tell your friends.
ReplyDelete