SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu
wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa
mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo
hayo kila baada ya miezi mitatu
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. DOTTO JAMES amesema kuwa uamuzi huo
umetolewa baada ya kupitia na kujadili mapendekezo ya baadhi ya wastaafu
waliofika Makao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha Jijini Da ers salaam
mwezi uliopita wakitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuwalipa kila
baada ya miezi mitatu mitatu ili waweze kujikimu kimaisha.
James
amesema kuwa Wizara imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wastaafu
kutaka kulipwa kila baada ya kipindi hicho huku wengine wakitaka kulipwa
kila mwezi hatua ambayo imeifanya Serikali kuamua kulifanyia kazi suala
hilo kwa kina na kuahidi kulitolea uamuzi hapo baadae.
Benny Mwaipaja, Msemaji Wizara ya Fedhana Mipango
Hawa Wastaafu hata akili zao zimestaafu. Pesheni duniani kote inalipwa kila mwezi. Kama huwezi kutunza wewe mwenyewe unadhani Serikali kukulipa kila miezi mitatu ndio una save? Si uende Benki Mara moja kila baada ya miezi mitatu ama hata baada ya mwaka utazikuta fedha zako? Ya nini kuwasumbua wanaotaka kulipwa kila mwezi. Hivi kweli viongozi wa Serikali wanao muda wa kushughulika na watu kama hawa?
ReplyDeletehii ni sawa ila kuna wastaafu mpaka wafike bank zipo mbali kiukweli wangeangalia wanaoweza kupewa mwezi wapewe
ReplyDelete