Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini Bw. Henry Tzamburakis cheti cha kutambua mchango mkubwa wa udhamini unaotolewa na kampuni hiyo katika kuadhimisha wiki ya Usalama barabarani jijini Arusha.
Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wakitazama bidhaa za Vodacom katika banda la Vodacom Tanzania kwenye wiki ya Usalama barabarabani inayoadhimishwa jijini Arusha.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam Mhe. Felix Lyaviva akisalimiana na makamanda wa polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, viongozi wa dini na wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika viwanja vya Mwembe Yanga.
Kamanda wa polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Temeke, (RTO) ASP Solomon Mwangamilo akitoa maelekezo.
Wanafunzi wa sekondari wakishiriki maandamano ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke.
Mbona wahandisi wa barabara na wahandisi wa mwendo na ajali hawahusishwi. Rungu hariwezi kuondoa vifo hivi.
ReplyDelete