Kanisa
la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la Mufindi limekabidhi zaidi ya shilingi milioni 02 kwa Mkuu wa wilaya ya Mufindi ikiwa ni
sadaka maalum iliyotolewa na waumini wa kanisa hilo kwa wahanga wa janga la
tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera mnamo septemba 13 mwaka huu.
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa
vyombo vya habari, imeeleza kuwa, msaada huo wenye jumla ya shilingi milioni 02 laki 02 na 52 elfu, umewasilishwa na mkuu wa
jimbo la Mufindi mchungaji Anthony Kipangula wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya Bomani mjini Mafinga.
Mchungaji
Kipangula amesema wakati wa mkutano wao wa jimbo ulioketi mapema mwezi oktoba, kwa kauli moja walikubaliana kutoa sadaka maalum kwa lengo la kusaidia waathirika wa janga hilo kubwa na lakihistoria hapa
nchini.
Akitoa
shukrani mara baada ya kupokea misaada hiyo kwa niaba ya serikali, Mkuu wa
wilaya ya Mufindi Jamhuri William, amewashukuru waumini wote waliojitoa kwa
sadaka hiyo maalum kwa ajili ya waathirika wa Kagera na kuahidi kuikabidhi kwa
Mkuu wa Mkoa, kisha akaziomba taasisi za dini ziendelee kuisadia serikali na
jamii kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kijamii.
Mkuu wa jimbo la KKKT la Mufindi mchungaji Anthony Kipangula (kati) akiongea na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya Bomani mjini Mafinga.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William akishukuru kwa msaada huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...