Na Dotto Mwaibale
MWALIMU Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula wa Shule ya Msingi Kumbukumbu katika Manispaa ya Kinondoni (pichani kulia) amefariki dunia wakati akiwa katika mkutano wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) na viongozi wa Idara ya Elimu wa manispaa hiyo.

Kifo cha mwalimu huyo kimetokea Desemba 1, 2016 Siku ya Ijumaa majira ya jioni wakati viongozi hao walipokuwa wakimalizia ziara yao ya kutembelea shule mbalimbali katika manispaa hiyo.
Mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula (pichani kushoto) alisema mke wake hakuwa na tatitizo lolote la kiafya na siku ya tukio hilo aliamka salama na kumuaga kuwa anawahi kwenye mkutano huo.

"Siku chache kabla ya kifo chake mke wangu aliniambia alikuwa hajisikii vizuri kwani alikuwa na uchovu wa kawaida" alisema Mwakatumbula.
Mwakatumbula alisema alipigiwa siku na kuambiwa kuwa mke wake alianguka ghafla wakati mkutano ukiendelea na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mount Mkombozi iliyopo maeneo ya Morocco ambapo waliambiwa tayari alikuwa amefariki.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa maziko yatakayofanyika leo marehemu ameacha mume na watoto watatu, Nico, Kelvin na Gloria.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Pole sana mzee Mwaka pamoja na walimu wote kwa ujumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...