Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto),  akimwelezea jambo Makamu wa Rais wa Shirika la  Serikali ya Japan, linaloshughulikia uratibu wa misaada ya maendeleo ya kimataifa, (JICA), Suzuki Noriko,  kuhusu hatua iliyofikiwa na TANESCO katika uboreshaji wa miundombinu ya kupoza na kusambaza umeme alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambapo JICA inashirikana na serikali katika kukiboresha kituo hicho.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Makamu wa Rais wa Shirika la Serikali ya Japan linaloratibu Misada ya Maendeleo laKimataifa (JICA), Bw. Suzuki Noriko ametembelea kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini kinachoendeshwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Ziara hiyo aliifanya Desemba 9, 2016 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba, alimtembeza kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uboreshaji miundombinu ya TANESCO ikiwemo jingo na mitambo.
Jengo jipya la kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambacho JICA imechangia ujenzi wake.
Ziara hiyo inakuja mwezi mmoja tu baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, kuzindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho cha Ilala, ni sehemu ya mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye jiji hilo.
JICA na mashirika mengine ya kimataifa yanafadhili mradi huo wa uboreshaji umeme jijini ambapo lengo ni kuwapatia wakazi wa jiji umeme ulio bora na wa uhakika zaidi, ambapo utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na kwa kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita 6.67.
Mhandisi Mramba, akiongoza ujumbe wa JAICA kutembelea kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...