SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.
SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.
SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ili kumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo yenye lengo la kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.  
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
 Mhandisi wa umeme wa TANESCO akiwa kazini jijini Dar es Salaam



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...