Na Anthony John,Globu Jamii.
Kampuni inayojishughulisha na Uhifadhi wa Mazingira na Usafishaji ya Green WastePro Ltd imesema kuwa, wamejitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya mfano na ya kisasa katika Jiji la Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni hiyo,Abdallah Mbena leo wakati akizungumza na Globu ya Jamii,amesema wamejitolea kutengeneza Garden hiyo ili kuunga mkono kampeni mbali mbali za Usafi zinazo ongozwa na Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa.
"Baada ya kuona kampeni mbali mbali za Usafi zinaendelea tukaona njia rahisi ya kuunga mkono kampeni hizo ni kujitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya kisasa katika jiji la Dar es salaam kwa kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano," amesema Mbena
Pia Mbena amesema mpaka itakapofika Mwezi wa tatu marekebisho hayo yatakuwa yamesha kamilika na tutakuwa tayari kuzindua.
Amesema kuwa "Watu wenge wamekuwa wakijiuliza maswali kwa nini pamezungushiwa uzio katika Sanamu la Askari Monument Garden lakini ni Kwa sababu tunataka kuiweka kuwa ya kisasa zaidi."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...