Na Zainab Nyamka, 

Globu ya Jamii

Timu ya Azam imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Cosmopolitan inayoshiriki ligi daraja la pili.
Azam wamewaondoa  Cosmopolitan katika michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ilichukua muda kwa Azam kuandika goli la kwanza mpaka  kipindi cha pili  baada ya John Bocco kutumia uzembe wa goli kipa ndani ya kumi na nane na mpira kumbabatiza na kurudi golini kwenye dakika ya 69.
Haikuchukua mda sana  Shaban Idd akitumia pasi safi iliyopigwa na John Bocco ikiwa ni uzembe pia wa golikipa na kuiandikia Azam goli la pili dakika ya 76,  Cosmo wakiendelea kujitutumua angalau kurejesha matumaini kwa kikosi chao ya dakika ya 79 Fidelisi Kyangu anaipatia timu yake goli la kufutia machozi akiunganisha mpira wa kona.
Dakika ya 80 Joseph Mahundi akiwa peke yake aliweza kuiandikia Azam goli la tatu na la ushindi na kuzima kabisa matumaini ya Cosmo.
Kwa ushindi huo kwenye mchezo wa Raundi ya Tano, Azam FC inaungana na vigogo Simba na Yanga kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
Yanga iliitoa Ashanti United kwa mabao 4-1 Jumamosi wakati Simba jana iliitoa Polisi Dar kwa mabao 2-0, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Baada ya mchezo huo, Azam FC inakwenda kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk73, Himid Mao, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mohammed na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Cosmopolitan; George Kijombi, Ramadhan Yusuph, Maulid Jumanne, Abdul Kussy, Fidelis Kyangu, Salum Hamisi, Hassan Mussa/Hafidh Hamisi dk62, Omary Hamisi, Ally Kabunda, Nuru Thabit na Fakhi Rashid.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...