Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
BARAZA la
Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko limemsimamisha kwa muda Diwani wa
kata ya Gwalama Elia Kanjero (CHADEMA),kutohudhuria kikao kimoja cha Baraza la
madiwani, kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali na
Madiwani.
Adhabu hiyo ilitolewa jana katika kikao cha baraza la madiwani la
halmashauri hiyo, ambapo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Maganga
alisema adhabu hiyo imetolewa na kamati ya maadili ya baraza hilo ili
kujenga nidhamu kwa madiwani wengine kuwa na nidhamu kama viongozi wanao
waongoza Wananchi.
Maganga alisema kosa moja wapo lilopelekea
adhabu hiyo ni pamoja na Diwani huyo kwenda kutolea ufafanuzi katika
kipindi cha kipimajoto cha ITV wa Rasimu ya kodi ya majengo ambayo
ilikuwa haijapitishwa katika halmashauri hiyo na kudai sheria hiyo
inayowakandamiza Wananchi bila kibali cha mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo.
Alisema Katika adhabu hiyo imeshuhudiwa na Mwenyekiti wa
halmashauri pamoja na Katibu wake ambae ni Mkurugenzi wa halmashauri na
Mtuhumiwa atakabidhiwa barua yake ya adhabu kupitia kwa Afisa utumishi
wa halmashauri.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwarama Elia
Kanjero(CHADEMA) alisema yeye kama kiongozi wa uponzani kuadhibiwa
kwasababu ya Wananchi ni faraja kwangu na nitaendelea kuwatetea Wananchi
kwa uwezo wangu na nitaitumikia adhabu hiyo.
Kanjero alisema
kosa lililopelekea kuadhibiwa ni pamoja na kuwashawishi madiwani kupinga
rasimu ya Wananchi kulipa kodi ya majengo pamoja na kwenda kutoa maoni
dhidi ya kutoshirikishwa Wananchi katika Baadhi ya mambo yanayo endelea
katika halmashauri, jambo ambalo sioni kama ni kosa la kunifanya
niadhibiwe.
"Suala lingine lililopelekea Kuadhibiwa ni baada ya
Mtendaji wa kata ya Garama kugushi saini yake na kusaini fedha za Mfuko
wa maendeleo ya kata baada ya kuleta malalamiko kwa Mkurugenzi
wamuhamishi ikawa chanzo cha Mimi kuonekana sina nidhamu suala ambalo
nilikuwa nikipigania haki yangu na Wananchi walio nichagua",alisema
Kanjero.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...