Na Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi
katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu
katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji Umbali wa
Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.
Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu aliagiza kusogezwa kwa
mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo
akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo
walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali
wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa katika ziara
ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika
uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchikuchoma mashine hizo bila
kujali mazao ambayo tayari yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama
zilizotumika kununua mashine hizo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa wilaya ya Karatu katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Katika
Kikao kingine Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wazee
wa Karatu pamoja na viongozi wa dini.
Mtaalamu
wa Halmashauri ya Karatu(kwanza kulia) akiwaandikisha Wananchi wa Kijiji cha Oldeani waliojiunga na
Mfuko wa afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza
kulia) akichangia Fedha kwa ajili ya wazee 10 kujiunga na Mfuko wa Afya ya
Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...