Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni vyema wananchi wakaanza kuwapuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakigeuza matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa. 

Hayo yamesemwa na katibu wa Siasa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. 

“CCM haitashiriki malumbano yasiyo kuwa na tija kwa lengo la kuleta uchochezi kwa wananchi kama ilivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani nchini, ambao wamekuwa wakitoa matamko kuwa Taifa limekumbwa na baa la njaa kama sehemu yao ya mtaji wa kisiasa, jambo ambalo Chama cha Mapinduzi kinaona hiyo ni siasa chafu” amesema Polepole.
Amesema kuwa kwanza tuwapuuze na maneno yao, kwani mwenye mamlaka ya kutangaza baa la njaa nchini ni Rais peke yake, hivyo ni vema wakajua kuwa Tanzania hatujafikia kiwango hicho, ambao wao wanakiomba, bali wanatakiwa kujua kuwa mpaka sasa tuna kiasi cha Tani Milioni 1 na nusu ambacho kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu wa chakula. 

Ameongeza kuwa sera ya CCM ni kujitegemea, hivyo kama ndicho chama ambacho kinaongoza dola,hatujafikia hatua ya kukosa chakula katika nchi yetu. 

Pole Pole Ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha kubweteka na kuwalaghai na kuwafarakanisha Wananchi,bali wanapaswa kuwaambia ukweli wananchi ili waweze kutunza nafaka na kuacha kutumia kwa matumizi mabaya kama kupikia pombe na masuala mengine yasiyokuwa ya lazima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...