Na Mwandishi Maalum, Davos, Uswisi
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
Baraza la Kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi duniani. Wajumbe hao ni wafuatao:
1. Bill Gates- Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation
2. Ray Chambers- Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria
3. Peter Chermin-Mwanzilishi wa Chermin  Entertainment na Chermin Group
4. Aliko Dangote- Rais na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group
5. Mhe. Idrisa Deby-Rais wa Chad kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taasisi ya ALMA
6. Mhe. Jakaya Kikwete-Rais Mstaafu wa Tanzania
7. Mhe.Graca Machel- Mwanzilishi wa Foundation for Community Development,Msumbiji
8. Luis Alberto Moreno-Rais wa Inter-American Development Bank
9.Mhe. Ellen Johnson Sirleaf- Rais wa Liberia.

Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030. Kuanzishwa kwa Baraza hilo kumetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika vita dhidi ya malaria katika miaka 15 iliyopita katika kupunguza vifo na maambukizi ya Malaria duniani kama ilivyoripotiwa na Ripoti ya MalariaDuniani ya mwaka 2016 ya Shirika la Afya Duniani. Msingi wa mafanikio hayo ndio chachu ya jitihada mpya za kutokomeza Malaria duniani ifikapo 2030.

Katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Davos, Baraza hilo limejadili kuhusu upatikanaji wa rasilimali za kutosha za kuwezesha kutoa msukumo katika upatikanaji wa vifaa tiba, dawa, tafiti na uvumbuzi wa mbinu na nyenzo za kisasa za kuzuia, kupambana na hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Malaria katika nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Baraza hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye utotoni kwake alipoteza kaka yake kwa ugonjwa wa  Malaria pamoja na ndugu wengine wengi kaika maisha yake amesema, " Kutokomeza Malaria iliwahi kuwa ndoto isiyotekeleza, lakini sasa kuifikia ndoto hiyo ni dhahiri.....tunawea kuifanya Malaria kuwa historia na kuutokomeza ugonjwa huu katili katika uso wa dunia".

Tanzania ni moja ya nchi zinazosifika barani Afrika na duniani kwa kuweza kupiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya malaria yamepungua kwa asilimia 70 na vifo vimepungua kwa asilimia 50.
Kwa habari zaidi fuatilia kwenye www.endmalariacouncil.org

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Ray Chambers ambaye ni  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria  katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Aliko Dangote na Bill Gates katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Bw. Bill Gates akisalimiana na Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Bw. Bill Gates,  Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation, katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...