Na Estom Sanga - Pemba.
Kamati ya
Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa imetembelea miradi
inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Unguja na Pemba na kuridhishwa
na hatua ya Maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba akizungumza na
wananchi wa shehia ya Ndagoni Kisiwani Pemba baada ya kukagua ujenzi wa tuta la
kuzuia maji chumvi ya baharini yasiathiri mashamba ya wananchi, ametaka
walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutumia fursa ya Mpango huo kupunguza
kero ya umaskini.
Ametoa Mfano
wa Miradi iliyojengwa kwa ufanisi kuwa ni pamoja na matuta ya kuzuia maji
chumvi ,upandaji wa mikoko, uchimbaji wa mitaro ya maji ,uundwaji wa vikundi
vya kuweka akiba, na ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati miradi iliyotekelezwa
na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa utaratibu wa ajira ya muda
kisiwani Unguja na Pemba.
Kwa
kutengeneza matuta ya kuzuia maji ya chumvi, walengwa hao wa TASAF wameweza
kuokoa zaidi ya hekta 200 za mashamba ya mpunga katika shehia ya Ndagoni
kisiwani Pemba kwa njia ya ushiriki kwenye ajira ya muda .
Kwa Upande
wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema serikali inafuatilia kwa karibu
utekelezaji wa shughuli za TASAF ili kuziboresha zaidi kwa manufaa ya wananchi.
Aidha Waziri
huyo ameiagiza TASAF kuviimarisha zaidi vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza vipatavyo 876 kwenye shehia 78 vilivyoundwa
na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kisiwani humo kwa kuvipatia
nyenzo muhimu hususani elimu na vitendea kazi ili vikundi hivyo viwe endelevu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF .
Matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko na uchimbaji wa mitaro ya maji ni Moja ya Miradi iliyojengwa kwa ufanisi Mkubwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo mbalimbali alipokuwa akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...