JANUARY 16, 2017 — MJI MKONGWE, ZANZIBAR: Harakati
za kukamilisha taratibu za ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band
hazikufanikiwa kutokana na changamoto za ugumu wa mawasiliano baina ya
uongozi wa kikundi hicho na Uongozi wa Sauti za Busara. Sauti za Busara
imesitisha taratibu za kuruhusu ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band
kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyotangazwa awali.
Yusuf
Mahmoud, Mkurugenzi wa tamasha amesikitishwa na ugumu wa kufanya
mawasilaino ndani ya muda husika kutengeneza mazingira mepesi ya
uandaaji wa taratibu zote za kuhakikisha kikundi hicho kinakamilisha
mahitaji yote ndani ya muda uliopangwa.
“Kuna
vipaji vingi sana vya muziki Tanzania. Vipaji hivi hufifia kwa sababu
ya uhaba wa ujuzi kwa mameneja ambao hawajibu barua pepe, wanakataa
kusaini mikataba, hawafiki kwenye mikutano hata baada ya kuthibitisha
kuwa watashiriki, na hawapokei simu,’’ Yusuf alikaririwa akisema hayo
wiki iliyopita kwenye gazeti la Sunday News.
Journey
Ramadhan, Meneja wa tamasha amesema kuwa jitihada za makusudi za
kuhakikisha Yamoto Band wanashiriki tamasha hazikuzaa matunda baada ya
yeye kufika Dar es Salaam na kumsubiri meneja wa Yamoto Band afike kwa
ajili ya maongezi lakini alisema yuko nje ya mji na asingeweza kuonana
naye.
“Ili
kuibua, kung’arisha na kukuza vipaji vya muziki Tanzania tunahitaji
mameneja wenye kuheshimu mawasiliano yatakayowezesha wanamuziki kupata
nafasi ya kuonesha vipaji vyao kupitia wadau wa muziki nchini. Pia ni
vema msanii apate naasi ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataia ni
lazima aanye mawasiliano kwa njia ya kieletroniki,’’ amesema Ramadhan.
Uzoefu
wa kufanya kazi na mameneja wa wanamuziki tofauti hapa nchini
unaonesha ugumu wa kupokea simu, kushindwa kujibu barua pepe,
kuhundhuria kwenye mikutano baina ya wadau wa muziki ili kujadili njia
sahihi za kuhakikisha wasanii wanapata nafasi ya ushiriki ni changamoto
kubwa zinazorudisha nyuma harakati za kukuza muziki Tanzania, amesema
Ramadhan.
Yusuf
ametoa wito kwa wasanii na mameneja wao kutumia tamasha la SzB ambayo
ni nafasi pekee na sahihi ya kutangaza na kuonesha kazi zao na kupanua
wigo wa kung’arisha taaluma zao na kuongeza mawasiliano na wasanii na
wadau wa muziki kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao hukutana kwenye
tamasha hilo la siku nne mfululizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...