Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Usalama Barabarani kimesema hakitaacha kuwachukulia hatua madereva watakaokiuka sheria za usalama barabaani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali barabarani.

Hayo yamesemwa  leo na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga wakati akifungua semina ya madereva iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani  RSA iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mpinga amesema ajali zinapoteza watanzania pamoja na wengine kuwaacha na ulemavu wa kudumu na taifa kukosa nguvu kazi ya kujenga uchumi.

Amesema madereva wa mabasi ndio wanachangia sehemu kubwa ya ajali ambazo nyingi zinatokana na makosa ya kibinamu hivyo kupitia kampeni ya Abiria Paza Sauti ilete matokeo ya kupunguza ajali.

Nae Mwenyekiti wa RSA, John Seka amesema semina ya madereva ni mwendelezo wa kampeni ya abiria paza sauti yenye tija kuwaongezea maarifa wanapokuwa katika kazi ya udereva.

Amesema RSA imedhamiria kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha ajali zinapungua nchini  na kuwa Tanzania bila ajali inawezekana.

Kwa Upande wa Meneja wa Usalama Barabarani  na Mazingira wa Sumatra, Geoffrey Silanda amesema wamefunga vidhibiti mwendo kwa mabasi 100 ya kanda ya ziwa kutokana na ukanda huo kuwa na ajali nyingi.

Amesema wataendelea kufanga mabasi yote vidhibiti mwendo ikiwa nia ya kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza watanzania wengi na wengine kuachwa na uemavu wa kudumu.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi Polisi (DCP), Mohamed Mpinga akizungumza na madereva wa mabasi yaendayo mkoani wakati akifungua semina ya madereva iliyoandaliwa Mabalozi wa Usalama Barabarani RSA iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa RSA, John Seka akizungumza katika semina ya madereva walioiandaa kwa ajili ya kuwaongezea maarifa wanakuwa safarini iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Usalama Barabarani na Mazingira wa Sumatra, Geoffrey Silanda akizungumza katika semina ya madereva wa mabasi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi Polisi (DCP), Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RSA, pamoja na madereva.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...