Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa vitanda vitano vya kujifungulia wakina mama wajawazito kwa hospitali ya Wilaya ya Mafia ili iweze kuwasaidia katika visiwa hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Muuguzi msaidizi wa hospitali hiyo, Agnes Mtawa amesema kuwa vitanda hivyo ni sehemu ya vitanda 20 vitakavyotolewana na hospitali hiyo kwa hospitali mbalimbali.

“vitanda hivi ni vile ambavyo vimekarabatiwa hapa hapa hospitali ambavyo vilikuwa vimeharibika na kwa bahati nzuri tukapata fursa ya kupewa vitanda na wahisani hivyo hivi ambavyo vilikuwa vimeharibika tunavitengeneza na kuvigawa katika hospitali zilizoomba”amesema Mtawa.

Ameongeza kuwa gharama ya kitanda kipya cha kujifungulia kinaanzia shilingi milioni moja na laki tano mpaka milioni moja na laki mbili hivyo ukarabati wa vyombo hivi unasaidia gharama za ununuzi wa vitu vipya.

Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali ambao wana uwezo kuanza kusaidia hsopitali zetukatika upande wa vifaa tiba.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akikabidhi vitanda vitano kwa Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai. Vitanda hivyo vimetatumika kwa kina mama wakati wa kujifungua.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Bi. Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vitanda hivyo.
Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...