Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wao Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwalaki Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan wakipiga ngoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwazawadia Kinyago cha Umoja na Mchoro wa Mlima Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mama  Emine Erdogan wakipeana mikono baada ya maongezi  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea baada ya yeye na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli ushuhudia uwekaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Uturuki Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na akiongea katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe  Magufuli katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe  Magufuli wakishuhudia ubadilishanaji hati baada ya kusaini baina ya mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa sekta binafsi Dkt Reginald Mengi na kiongozi wa msafara wa wafanyabiashara wa Uturuki katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.

PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MHE.RAIS JPM TUNAOMBA UTUSIKILIZE HATA SISI WAFANYABIASHARA YA VIUMBE HAI TUNAONEWA NA KUDHULUMIWA HAKI ZETU,Tunasikitika kusema kuwa Tanzania ni nchi ya ajabu.nchi inayodhamini wageni kuliko wazawa nasema hivyo kwa masikitiko makubwa kuwa biashara yetu ya viumbe hai imefungwa na Waziri wa Maliasili na Utalii bila kujali hasara na umasikini ambao tumeingizwa.Wafanya biashara hawa wamelipia kila kitu wanavibali ,leseni halali inasikitisha kwa nini? tunanyanyaswa katika nchi yetu wenyewe ,Nasikitika kusema kuwa kuna mrusi ndiye aliyesababisha hii hali kisa soko la ngedere.mrusi huyu zaidi ya kujifanya anazalisha wanyama kutokana na wale alioingiza kutoka South Africa lakini ukweli amekamata watoto wa wanyama hao na kujifanya kazalisha si kweli nchi inaibiwa tunaomba DNA test ifanyike kwa wanyama wote walioko katika stock yake ,mtaona udanganyifu alioufanya.Waziri kwa interest zake anambeba huyu mgeni bila kujali kuwa anaidanganya hata serikali yake kuwa wanyama hawa wanatoroshwa wakati si kweli.Tumbili waliokamatwa kwenye uwanja wa KIA.walikuwa na vibali halali kapotosha ukweli kwa interest zake hata mahakama imethibitisha hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...