Na Anthony John Glob jamii.

Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali.

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.

''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama muhuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema

Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.

Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi. 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizungumza na wawakilishi kutoka serikali za mitaa leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kusitisha muongozo wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizungumza akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wawakilishi kutoka serikali za mitaa wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene wakati akisitisha muongozo wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serika.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizunguimza akizungumza na waandishi wa habari.
Wawakilishi kutoka serikali za mitaa wakisikiliza jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene wakati.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka serikali za mitaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...