Mkurugenzi
wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza
kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye
uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.
Ntetema
amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza
ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha
ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino
waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.
Mwasisi
wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash,
ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye
ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa
ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye
ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani
Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya
ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu
zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza.
Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau kuhusu ualibino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.
Binagi Media Group
Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa
Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...