Ushauri umetolewa kwa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) kuangalia namna ya
kuwaendeleza wachezaji wanaohudhuria kliniki ya wiki moja ya Airtel Risingf Stars inayofanyika
kwenye uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Ushauri huo umetolewa na Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars Edna
Lema ambaye ni moja kati ya makocha wanaotoa mafunzo kwa wachezaji hao ambao
walichanguliwa kutokana na michuano ya awamu ya sita ya Airtel Rising Stars.
Tuna wachezaji wazuri na wenye vipaji vya hali ya juu na kliniki hii inadhirihisha hivyo. Kwa
wachezaji hawa kuendelea na vipaji vyao ni lazima kuwe na mipango endelevu. Kinachofanyika
kwa sasa ni kwamba baada ya kliniki hii, wachezaji wataruhusiwa kurudi makwao mpaka pale
tutakapokuwa na michuano ya kimataifa ndio tuanze kuwatafuta bila kujali huko walikokuwa
walikuwa wanafanya nini. Bila kubadilisha hali hiyo ni vigumu kwa timu zetu kupata mafanikio,
alisema Lema.
Tuliendea kufanya ziara nchini Cameroon na kushuhudia mipango yao ya kuendeleza vipaji.
Kwao wanakuwa na kliniki za kudumu za wachezaji wa rika zote. Kwa kuwaweka wachezaji
pamoja ujenga hali ya ukaribu kati yao pamoja na makocha pia na kwa hali hiyo sio ajabu kwa
nchi hiyo kuwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia na hile ya Afrika. Natoa wito kwa TFF
kubadilisha jinsi ya kutunza wachezaji wetu kuleta mafanikio kwenye timu zetu za taifa,
aliongeza Lema.
Akiongelea kuhusu kliniki ya Airtel Rising Stars, kocha huyo Msaidizi wa Twiga stars alisema
anaamini timu ijayo itakuwa na vipaji vya hali ya juu. Wachezaji hawa ni wazuri sana, ukipewa
jukumu ya kuchangia timu inaweza kuwa mtihani umchukue yupi na kuwacha yupi. Kwakweli
tunafurahi kupata vipaji hivi kutoka kwenye mashindano haya.
Lema alitoa pongezi kwa kampuni ya Airtel kuwa na program hii ya vijana ambayo kwa mwaka
jana iliweza kufika mikoa tisa ya Tanzania. ‘Hii ndio njia bora na sahihi ya kupata wachezaji wa
timu zetu, alisema Lema.
Mmoja ya wasichana wanaoshiriki kwenye kliniki hiyo Eva Willes alisema anayo furaha ya kuwa
mmoja ya washiriki wa kliniki hiyo. Kwa muda mrefu nimekuwa nikicheza mpira wa miguu na
nilikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa timu ya taifa. Kuwepo kwenye kliniki kunanifungulia
milango ya kutimiza ndoto zangu. Nitaendelea kuongeza bidii pamoja na kuwasikiliza makocha
kwa makini nipate mafanikio zaid, alisema Willes.
Kocha Mkuu wa Timu ya Wasichana U-17, Sebastian Nkoma
akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa Kliniki
ya Airtel Rising Stars yanayofanyika katika Uwanja wa Jakwaya
Kikwete Dar es Salaam jana kutafuta vijana wenye vipaji kuunda
Timu ya Taifa.
Kocha Msaidizi wa Timu ya Wasichana ya Twiga Stars, Edna
Lema akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa
kliniki ya Airtel Rising Stars yanayofanyika katika Uwanja wa
Jakwaya Kikwete Dar es Salaam jana kutafuta vijana wenye
vipaji kuunda Timu ya Taifa.
Wachezaji wa Timu ya wasichana U-17, wakifanya mazoezi
katika Uwanja wa Jakaya Kikwete wakati wa Kliniki ya Airtel
Rising Stars Dar Salaam jana kutafuta vijana wenye vipaji
kuunda Timu ya Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...