Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba serikali kupitia Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Umma ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa katika utumishi wa Umma.

Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Makao Makuu ya TPSC Mtaa wa Bibi Titi Jijini Dar es Salaam , Waziri Kairuki alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa watumishi hao.

Aliongeza kuwa pia serikali inakamilisha mchakato wa mandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini.Katika kuongeza ufanisi na tija wa chuo hicho, chuo kimejenga, kuhuisha na kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu.

“Baadhi ya mifumo hiyo ni mpango mkakati mwa mwaka 2016-2021,utekelezaji kikamilifu kwa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la malalamiko na kamati za uadilifu.Waziri alisema majukumu mengine ni kuendelea kusimika mifumo ya Tehema, miundombinu ya mtandao (LASN) , Mtandao wa serikali (Govnet) , mfumo wa simu za serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM).

Waziri Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa watumishi wa Umma katika utunzaji wa kumbukumbu na Uhazili, Chuo kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza katika maeneo hayo mawili.“Rasimu ya Mitaala hiyo, imeshaandaliwa na kuwasilishwa baraza la Ithibati na Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa.” 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki(kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Henry Mambo wakati alipokuwa akiwaelezea maadeleo ya ukarabati wa majengo ya chuo hicho tawi la Magogonijijini Dar es Slaam, kamati ya bunge ilifanya ziara ya kikazi katika chuo hicho jana. 
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.Henry Mambo, akisisitiza jambo mbelea ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza,anayefuata ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki na kwa kwanza kulia ni Suzan Mlawi, Naibu Katimu Mkuu wa Wizara hiyo ya Ofisi ya Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki (kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wakamati ya kudumu yabunge ya Utawala na Serikaliza Mitaa wakati walipofanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya chuo hicho,Mtaa wa Bibi Titi, jijini Dar es Salaam, jana .Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishiwa Umma Dkt.Henry Mambo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Ino Communications Barnabas Lugwisha, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki wakati wa ziara hiyo jana Chuo cha Utumishi wa Umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...