Na Greyson Mwase, Mwanza

Wananchi wa wilaya ya Ukerewe wameipongeza serikali kwa kasi ya miradi ya umeme katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi hususan za uvuvi.

Waliyasema hayo katika nyakati tofauti jana katika ziara ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini yenye lengo la kujionea hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya miradi hiyo inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu wa Kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank Matondane alisema kuwa kitongoji hicho hakikuwa na ndoto ya kupata umeme wangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika lakini matumaini yamepatikana baada ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya umeme katika kitongoji hicho kupitia kampuni ya Rex Energy.

Alisema mara baada ya wananchi kuhamasishwa na wataalam kutoka kampuni ya Rex Energy na kuona zoezi la ujenzi wa miundombinu ya umeme, walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutodai fidia hali iliyorahisisha utekelezaji wa mradi huo.

Matondane alisema kuwa mahitaji ya umeme katika kitongoji cha Ghana/Siza chenye wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya 2,500 hadi 5,000 ni makubwa husuan wavuvi wanaohitaji umeme kwa ajili ya kwenye majokofu ya kuhifadhia samaki.

Aliongeza kuwa shule pamoja na maduka ya madawa baridi yanahitaji umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, uchumi katika kisiwa hicho utakua kwa kasi kutokana na fursa zilizopo na kuvutia wawekezaji kwenye ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama ya samaki.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto mbele) akibadilishana mawazo na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kwenye ziara ya kuelekea katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.
Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply kilichopo Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Sitta Ngissa (katikati) akielezea hali ya uzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya jua katika kituo hicho, Kushoto ni David Mwakigonja kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Mfumo wa kuongozea mitambo na vifaa vya kuzalisha umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...