Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizindua Jiwe la Msingi la Kiwanda Keds.kwakushirikina na Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni (Keds) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.

Kiwanda hicho ni cha pili kujengwa katika Bara la Afrika baada ya cha kwanza kujengwa nchini Ghana.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo,Waziri Mwijage amesema kuwa amefurahi kuona mapambano yakuendeleza Tanzania ya Viwanda,amesema kupitia ujenzi wa Viwanda hivyo ukuaji wa Uchumi utakuwa sambamba na ukuaji wa Maendeleo ya Watu.

Pia amesema kuwa Kiwanda hiko cha Keds kimeitoa Tanzania kimasomaso katika kutimiza asilimia 40 ya upatikanaji wa ajira pamoja na kuziomba Mamlaka za Mikoa kote nchini kuiga Mfano wa Pwani katika Uwekezaji wa Viwanda na kujifunza ukarimu kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Clifford Tandari amesema kuwa ni fursa muhimu kwa kuwa Kampuni hiyo tayari ina Kiwanda Ghana hivyo kujengwa Tanzania kitakuwa cha pili.

Amesema kuwa baada ya Kiwanda hicho kuisha kitaokoa gharama za uingizaji wa sabuni kutoka nje.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng,amesema tangu kuanza kwa mradi huo wametumia muda mfupi kuweka sawa ardhi ya eneo hilo pia amesema kuwa watajenga kwa uzoefu na ujuzi ili kutimiza azma ya uwekezaji bora Tanzania.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa Kiwanda cha Keds kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini, Clifford Tandari akizungumza wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng akizungumza wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Baadhi ya viongozi mbalimbali na wanachi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni(Keds) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...