Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya Yanga  imeandika barua Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo kuomba iruhusiwe kuanzia wikiendi hii kutumia Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru mjini Dar es Salaam kwa mechi zake za mashindano ya nyumbani.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kuwa wameandika maombi hayo kwa lengo la kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa kwa michezo yao ya ligi kuu ili wachezaji waanze kuuzoea kelekea mtanange wao wa  michuano ya Afrika, ambayo watatumia Uwanja wa Taifa.

Kwa sababu hiyo, Baraka alisema wanataka waruhusiwe kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa, ili wauzoeee mapema hata mechi zao za michuano ya Afrka itakapoanza wawe tayari.

“Kama unavyojua kwa muda mrefu hatujautumia Uwanja wa wetu huu kipenzi wa Taifa baada ya kuzuiwa na Serikali kufuatia vurugu za kwenye mechi yetu na Simba baada ya mashabiki wa wenzetu kufanya fujo na kuvunja viti,”.

“Lakini tutambue kuwa tuliingia mkataba maalum na Serikali wa kuutumia Uwanja huu kwa mechi za mashindano ya Afrika na ule wa Uhuru kwa Ligi Kuu pekee na  kwa kuwa tunakaribia kuanza mechi za Klabu Bingwa  Afrika tunaiomba Serikali ituruhusu kuhamishia mechi zetu za mashindano ya nyumbani Uwanja wa Taifa, ili iwe sehemu ya maandalizi yetu ya michuano hiyo ya Afrika,”amesema Baraka.

Yanga watashuka dimbani dhidi ya Mwadui  mechi itakayochezwa Januari 29 Jumapili Jijini  Dar es Salaam na Februari 05 wataikaribisha Stand United Februari 5 na kisha kuanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Ngaya De Mbe.

Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya De Mbe kutoka visiwa vya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Picha ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akikabidhiana mkataba Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  kwa makubaliano ya kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...