Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wahanga wa Ajali ya kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa RZ uliopo katika Kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Mkoani Geita iliyotokea tarehe 26 Januari, 2017.

Aidha, Prof. Muhongo amewataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kuchukua hatua za haraka kusimamia mazoezi ya uokoaji pindi zinapotokea ajali migodini pasipo kusubiri miongozo ya Waziri.

Pia amewaagiza Makamishna hao kufanya ukaguzi katika migodi mikubwa na midogo katika maeneo nayo na kuongeza kuwa, zoezi hilo la ukaguzi linatakiwa kufanywa haraka.Pia amemtaka Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, kufuta leseni zote za uchimbaji madini ambazo hazifanyi kazi.

Akizungumzia kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo chini, Prof. Muhongo amesema kuwa, Sera na mipango ya Serikali ni kuwandeleza wachimbaji hao na kuhakikisha kuwa, wanatoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa Kati.

Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo ameitaka Migodi Mikubwa yote nchini kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na kueleza kuwa, migodi hiyo imepewa wiki 6 iwe imejiandikisha katika soko hilo.

Pia Prof. Muhongo amemshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkoa wa Geita, Viongozi wa Wizara, Wachimbaji na kampuni zote zilizoshiriki zoezi la uokoaji na kufanikiwa kuokolewa kwa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya Wahanga wa ajali ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ, Mkoani Geita. Prof. Muhongo alifika mgodini hapo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati) akimuongoza Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi wa dhahabu wa RZ.
Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
Wachimbaji wadogo wakimwonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake namna walivyookolewa baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa dhahabu wa RZ, uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi akiwaongoza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi ambako wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa wote wakiwa hai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...