Na Dotto Mwaibale

CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimefanikiwa kutoa falsafa ya kwanza ya Udaktari (PHD), licha ya changamoto ya utoaji elimu katika majengo ya kupanga kwa gharama kubwa.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam.

Alisema katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 499 wamefanikiwa kumaliza masomo yao kwenye fani mbalimbali, wanafunzi 45 ngazi ya cheti na Stashahada 47.

Wengine waliohitimu shahada 334,Shahada ya udhamiri 71 na shahada ya udamivu ni mmoja licha ya uongozi wa chuo hicho kukutana changamoto nyingi ndani ya miaka mitano lakini wanamshukuru mungu kwa hatua hiyo.

“Namshukuru mungu kwa kutupatia kibali cha kufikia hatua hii ya kufanya mahafali, lakini bado tumekuwa na changamoto ya majengo kwa bado tupo kwenye majengo ya kupanga,” alisema.
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho.
Mgeni rasmi Mheshimiwa Kificho (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi, Dk.Abdillah Chande, Dean Chuo cha Elimu, Dk.Mary Mosha, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Dk. Costa Mahalu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk.William Kudoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji mstaafu, Steven Bwana.
Wahitimu wa shahada ya kwanza katika ngazi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...