Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, itakuwa
mwenyeji wa Maadhimisho ya 11 ya ‘Siku ya Nile’ yatakayofanyika Dar es
Salaam, tarehe 22 Februari, 2017.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Sekretariati ya Nile
Basin Initiative (NBI)
itaandaa Maadhimisho ya 11 ya Siku ya Nile (Nile Day) yatakayofanyika tarehe 22 Februari, 2017 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Lengo la Siku ya Nile ni kukuza uelewa kwa watu wote
kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote wanachama, masuala
yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali
za Bonde la Mto huo.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni ‘Our Shared Nile: Source of Energy, Food and
Water for All’. Kauli mbiu hii inalenga kuonesha umma umuhimu wa Mto
Nile katika kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa chakula, maji, na nishati ya
umeme kwa jamii nzima na vilevile, kuonesha muingiliano uliopo katika sekta
husika kwa lengo la kuondoa umasikini, kuboresha maisha ya jamii na kuleta
maendeleo endelevu.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa ni Mhe. Samia Suluhu
Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washiriki takribani 600 watashiriki maadhimisho hayo zikiwemo sekta mbalimbali,
taasisi za kiserikali, taasisi zisizo za kiserikali, wadau wa
maendeleo na watu
mashuhuri.
Maadhimisho yanatarajiwa kuanza saa 02:30 asubuhi,
siku ya tarehe 22 Februari, 2017 kwa maandamano yatakayo ongozwa na Bendi ya
Polisi kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Ukumbi wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, ambapo maonesho na ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo yatafanyika.
KARIBUNI SANA!
Inj. Emmanuel
Kalobelo
KAIMU KATIBU MKUU
Wizara ya Maji
na Umwagiliaji
20 Februari,
2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...