Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.

“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.

Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya nchi yetu. ‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”
Wanahabari mkoa wa Iringa walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa.

Wanahabari mkoa wa Njombe walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa 
Wanahabari mkoa wa Ruvuma walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa 
Meneja mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu (TPDC) akitoa neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...