Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakifu  wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari  mkoani Dodoma katika  ukumbi wa Hazina  Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika kazi zao.
Mjadala huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
 Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila siku.
Wakili wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.
  Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...