KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya Mwenyekiti wake Alex Msama, amemtangaza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamaska la mwaka huu utakaofanyika April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuelezea maandalizi ya tukio hilo linalowaleta watu wengi bila kujali tofauti za dini zao kusikiliza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia nyimbo mbalimbali, Msama wao wamefurahi kuona Mama Samia amekubali kubeba jukumu hilo kwa mikono miwili.

Msama alisema pamoja na Mama Samia kukubali kubeba jukumu hilo lenye heshima na hadhi yake katika jamii, pia amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kumwakilisha kwani siku hiyo atakuwa nje ya nchi.

“Tunamshukuru Mama yetu Makamu wa Rais, Mama Samia kwa kukubali kubeba jukumu la Tamasha la Pasaka kwa sababu ni jambo kubwa kweyu sisi waandaaji. Kwa mikono miwili amekubali heshima hiyo, lakini kutiokana na siku hiyo atakuwa nje ya nchi, amemteua Waziri Mwigulu kumwakilisha,” alisema Msama.

Alisema baada ya Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kabla ya kwenda Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Iringa kwa tarehe zitakazotajwa kulingana na ratiba kamili.

Kuhusu waimbaji, Msama amesema waimbaji watatu kutoka Kenya, wamethibitisha kushiriki Tamasha hilo ambao ni mwimbaji mkongwe, Faustine Muhishi, Danny ‘M’ na Messi Masika ambao watashirikiana na wengine waliotajwa.
 
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi  wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi  wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...