Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza hilo. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wafungwa ambao wana ujuzi wa kujenga nadhani wapo Mtwara hata kama sio kwa gereza hio la Namajani. Kwanini wasitumike kujenga hata nyumba za matofali ya kuchoma kuboresha mazingira ya kuishi wafungwa pamoja na nyumba za askari magereza? mazingira yanayoonekana pichani ni duni sanaaaa yani hiyo nyumba wanayosema ya mmoja wa askari magereza yani hata haifanani na nyumba anayoishi mfanyakazi wa serikali anayelipwa mshahara. wakuu wa magereza kuweni wabunifu watumieni wafungwa kuboresha masuala mbalimbali ya magereza sio kulima na kufuga tu.
    Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...