Na Rhoda Ezekiel Kigoma,


KAMATI ya ulinzi na Usalama Wilayani Kasulu imeteketeza Shamba la bhangi hekari moja iliyo kuwa ikilimwa katika hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusini pamoja na kukamata Watuhumiwa wanne wawili wakiwa ni raia wa Burundi wakiwa wanatumiwa katika Kilimo cha hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali Marko Gaguti wakati wa kuteketeza shamba hilo, alisema kumekuwa na tabia ya wakulima wengi kulima bhangi pembezoni mwa mji wakichanganya na mazao Mengine, suala linalosababisha watoto wengi kuharibika na uharifu kuongezeka.

Gaguti alisema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Wananchi kwamba kuna mtu analima bhangi,Jeshi la polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ilifanya msako na kukamata shamba la Mkulima, Yotham Ngeze aliekuwa akiwatumia vibarua wanne wakiwemo warundi wawili na vijana wawili ambao walikuwa wakilima shamba hilo.

Aidha Gaguti aliwataka wakulima kuacha tabia ya kulima bhangi, zao ambalo ni haramu na badala yake watumie ardhi nzuri waliyo nayo kulima mazao ya chakula kutokana na hali ya upatikanaji wa chakula ulivyo kwa sasa, na kwa atakae kutwa analima zao hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake Serikali inamacho mengi wataendelea kuwafuatilia popote pale .


Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali Marko Gaguti akishiriki kuteketeza bhangi iliyokuwa imelimwa huku ikiwa imechanganywa na mazao mengine.

Zoezi la kuteketeza Bhangi likindelea
Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa wakiohojiwa na vyombo vya habari kufuatia kukamatwa kwa tuhuma za kulima Bhangi katika hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...