Na Mbaraka Kambona,
Ujumbe wa
Tume inayohamasisha umoja na mshikamano na kupambana na aina zote za utengano wa
Makabila kwa jamii ya watu wa Kenya ( National Cohesion and Integration
Commission) umesema kuwa wanatamani kuiona Kenya inakuwa kama Tanzania ambayo
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliijenga katika misingi ya
umoja na mshikamano.
Wakiongea
katika kikao kifupi baada ya ujumbe huo kufanya ziara katika ofisi za Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam,ujumbe
huo haukusita kueleza hisia zao juu ya Tanzania na kueleza kuwa suala la Ukabila nchini Kenya bado lipo na
ndio moja ya mambo ambayo wanashughulika nayo.
“Tungetamani
sana Kenya ingekuwa kama Tanzania, kwani Mwalimu aliijenga Tanzania kuwa taifa moja”
alisema Kamishna Dzoro, na kuongeza: “Tunasikia
wivu kwenu...Tanzania imejengwa kama Taifa sisi Kenya bado ni nchi”, aliongeza
Profesa Gitile
Naye,
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Nyanduga wakati akiwaeleza kuhusu majukumu ya
tume, pia aliwaomba kwamba, kwa kuwa
wanaelekea katika uchaguzi mkuu wahakikishe vyama vya nchini kwao vinajihepusha
na kuunda vikundi vya vijana wa chama “youth league” ambavyo kwa uzoefu
uliopatikana katika uchaguzi uliopita
nchini Tanzania vikundi hivyo vilianza
kujiingiza katika majukumu ambayo sio yao ya kutaka kulinda maeneo ya kupigia
kura na kulinda kura jambo ambalo ni hatari kwa
amani na usalama wa nchi.
Ujumbe huo
wa watu wanne ulioongozwa na Kamishna, Mhe. Morris Dzoro ulikuwa na lengo la
kujifunza namna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wanavyofanya kazi
zake.
Wajumbe wengine
waliokuwa katika ziara hiyo ni Kamishna,
Profesa Gitile Naituli, Mkurugenzi wa
Programu, Bi. Millicent Apondi Okatch na Afisa wa elimu ya uraia na
uhamasishaji, Ndugu Richard Nderitu.
NCIC
ilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha umoja na mshikamano katika jamii ya watu
wa Kenya kwa kuandaa michakato na sera
mbalimbali zinazowezesha kuondoa aina zote za ubaguzi wa kikabila nchini humo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Mukirya Nyanduga
(kulia) akiongea katika kikao kifupi na ujumbe wa Kamisheni inayohamasisha umoja kwa jamii ya watu wa
Kenya na kuondosha aina zote za utengano wa makabila (National Cohesion and
Integration Commission - NCIC) ya nchini Kenya uliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza namna tume inavyofanya
kazi zake. Ujumbe huo uliongozwa na Kamishna, Mhe. Morris Dzoro (kushoto), wa
pili kushoto ni Kamishna, Profesa Gitile Naituli, wa tatu kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Programu, Bi. Millicent Apondi Okatch.
Mkurugenzi
wa Programu, Bi. Millicent Apondi Okatch akiongea katika kikao kifupi baina ya
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na National Cohesion and
Integration Commission (NCIC), kulia anayeandika ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Mukirya Nyanduga.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (kulia) akiongea na Makamishna wa
NCIC mara baada ya kumaliza kikao. Kushoto ni Kamishna, Mhe. Morris Dzoro na
katikati ni Kamishna, Profesa Gitile Naituli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...