Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao (kulia) akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas (kushoto) akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao.
Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo) Bi. Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Maafisa Mawasiliano Serikalini
wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya Serikali kwa kuweka taarifa
mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa na taasisi hizo ili
kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.
Rai hiyo imetolewa
leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Dkt.
Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa tovuti za
Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani
humo.
Dkt. Bakari amesema
dhana ya Serikali Mtandao ni kuhuisha
matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi
hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana
na wakati ili kurahisisha upatikanaji wa
huduma hizo.
“Wakala kwa
kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali
kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti
zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...