SHIRIKA la ndege la Qatar (Qatar Airways) limeadhimisha miaka kumi ya kutoa huduma ya usafiri wa anga kati ya miji ya Dar es Salaam na Doha huko Mashariki ya Kati jijini jana. 

Sherehe hizo zilizofanyika zilihudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini.Shirika hilo lilianza kutoa huduma ya usafiri huo wa anga kati ya Dar es Salaam na Doha mwaka 2007 likitumia ndege aina ya Airbus 320.

Huduma hii ilipanuka zaidi miaka mitano badaye kwa shirika hilo kuanza kurusha ndege zake moja kwa moja kutoka kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro na badaye Zanzibar mwaka 2015 ili kukidhi mahitaji ya soko lililokuwa likikua kwa kasi.

Leo hii Qatar inatoa huduma za ndege zake zinazoruka kila siku moja kwa moja kutoka Dar es Salaam, Kilimanjaro and Zanzibar kupitia Doha na kupanuka kwenye miji zaidi ya 150 huko Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Pacific na miji muhimu kama vile London, Paris, Dubai, Shanghai na Beijing.

Mtendaji Mkuu wa shirika hili Ehab Amin, alisema: Qatar Airways ina furaha kuadhimisha miaka kumi ya huduma zake hapa nchini ambazo zinalipa shirika uwezo wa kutimiza haja ya kusafirisha watalii na wafanyabiashara katika eneo hili la Afrika ambalo lina vivutio vizuri na biashara kedekede. 
Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania,Basel Haydar, akizungumza alipokutana na waandishi wa habari katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam.
Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania Basel Haydar, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini, katika sherehe za Kutimiza miaka kumi (10) ya kutoa huduma nchini Tanzania.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa tasnia ya usafiri wa anga nchini Tanzania wakimsikiliza kwa makini meneja mahusiano ya umma (PR Manager) wa Qatar Airways Bi.Gayathri Pradeep alipokua akielezea jinsi Qatar Airways wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wateja wao.
Wageni (waandishi wa habari) na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga wa Qatar Airways Tanzania katika picha ya pamoja katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...