Timu ya Tanzania "Taifa Stars" imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Timu ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo uliochezwa leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa ilifanikiwa kutoka na ushindi huo baafa ya Mshambuliaji wa Kimataifa anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji Mbwana Samata kufunga magoli yote.

Dakika ya pili ya kipindi cha Kwanza Samata aliweza kuipatia Stars goli la kuongoza lililodumu mpaka mapumziko huku kila timu ikionekana kutafuta goli kwa udi na uvumba.

Kipindi cha pili kinaanza ambapo Botswana wanafanya mabadiliko lakini wanshindwa kutumia nafasi walizozipata.

Katika dakika ya 87, Mbwana Samata anaiandikia Stars goli la 2 kwa faulo ya nje ya 18 akiupiga mpira huo moja kwa moja ambapo mpala dakika 90 zinamalizika Stars 2-0 Botswana.

 Stars wanatarajiwa kucheza tena Jumanne dhidi ya Burundi ikiwa ni muendelezo wa mechi za kirafiki za kimataifa.
 Kiungo wa Timu ya Taifa Stars, Himid Mao akiruka juu sambmba na Beki wa Botswana kuwania mpira wa juu, katika Mchezo wa kirafiki wa rekodi za FIFA, uliochezwa jionu ya leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda bao 2-0.
 Beki wa kati wa Botswana , Mosha Galemonthale akimchezea vibaya Mbwana Sammata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Mbwana Ally Samatta  kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Botswana, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...