SERIKALI imesema ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Zinga Pharmaceuticals katika kitongoji cha Zinga mkoa wa Pwani utasaidia sana katima kupunguza gharama za ununuaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

Pia imesema gharama ambazo hutumia kwa mwaka kwa ajili ya ununuaji wa dawa kwa mwaka ni dola za kimarekani milioni 100.

Taarifa hiyo imetolewa na Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Siana Mapunjo kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa kiwanda cha dawa cha Zinga, uliofanyika Bagamoyo mkoani, Pwani leo.

Mapunjo amesema kutokana na gharama ambayo serikali hutumia kunulia dawa kwa mwaka inakadiriwa kuwa hadi ifikapo mwaka 2021 kiasi cha dola za Kimarekani 350 zitatumika kwa ajili ya ununuzi huo.

“ Hadi sasa nchini tuna viwanda vya dawa za binadamu 13 ambavyo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 na kuisababishia serikali kupoteza sh. milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa dawa,” alisema.

Amesema kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals kitasaidia kupata dawa muhimu kwa wakati na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Dkt. Mary Mayige alisema kiwanda hicho kitagharimu kiasi cha sh.bilioni 70 za Kitanzania na kutarajiwa kukamilika baada ya mwaka mmoja na nusu.

“Uzalishaji wa dawa za binadamu nchini bado ni upatikanaji wake kwa hospitali binafsi na serikali umeshuka kwa kiwango mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita kwa hiyo kupitia kiwanda hiki tutafikia malengo,” amesema.

Dk. Mayige alizitaja dawa zitakazotengenezwa kuwa ni dawa wa kufubaza makali ya virusi vya ukimwi, antibiotiki, dawa za maumivu, malaria, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, shinikizo la damu na kisukari.

Naye Mwakilishi tokaWizara ya Viwanda na Uwekezaji, Elly Pallangyo, amesema uwekezaji huo umejizatiti kuweka mazingira mazuri kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo. “ Hatutaweza kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda kama watu wake hawatakuwa na afya nzuri,” alisema.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa alisema atahakikisha anashirikiana na wawekezaji hao ili serikali iweze kutekeleza mradi huo kwa wakati.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Happyness Seneda alisema mkoa wa Pwani una jumla ya Viwanda vikubwa na vidogo 264 kati ya hivyo 88 ni vikubwa na kati, na ameahidi kwamba mkoa wa Pwani utatoa ushirikiano utakaotakiwa ili kufanikisha mradi huo ni mingine yote.

Mwakilishi wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto,Siana Mapunjo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Happyness William Seneda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha zinga Dkt.Mary Mayige akiwaeleza wageni mipangilio ya Zinga Pharmaceuticals watakavyotumia utaalam wao kuzalisha dawa nyingi za binadamu zenye viwango vya kimataifa hapa nchini.
Mshauli Mkuu wa kiwanda cha dawa za binadamu Zinga kutoka Ujerumani Mhandisi Bernt Kleinmann akifafanua jambo.
Wadau wa mradi katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.

Habari na picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...