Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika  Ukumbi wa HazinaMjini Dodoma 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizindua tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo  mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe. (Kushoto)  ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick wakifuatilia uzinduzi huo.
 Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene,  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali katika Mikoa na Halmashauri wakifuatilia uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika  jana Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina. Tovuti hizo zinalenga katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa haraka ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick akiongea katika uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...