Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imezindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma za kibenki zinazozingatia kanuni za kiislamu kwa njia ya simu ikiwa ni hatua ya kuboresha na kupanua huduma zake kwa wateja.

Katika hatua ya kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya simu, Zantel imeshirikiana na BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zote za kibenki kama vile kuweka au kutoa fedha, mikopo, kulipia ankara zao za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu n.k.

Akizindua huduma hizo leo (23/03/2017) kisiwani Pemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada alisema huduma hizo kutoka Zantel zimekuja katika wakati muafaka kwa wananchi wa Pemba na kuongeza kuwa yeye na Wizara yake wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mitandao mingine ya simu katika kuhakikisha huduma za simu zinaboreshwa zaidi visiwani humo.

“Uzinduzi wa huduma ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma ya kibenki kwa njia ya simu ni vitu ambavyo wananchi wa Pemba wamekua wakivisubiria kwa muda mrefu. Niipongeze Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kwa kulitambua jambo hili na kulifanyia kazi kwa haraka” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni yake katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao. 



Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakizindua huduma za mtandao wenye kasi zaidi wa 4G wa Zantel na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki hiyo kisiwani Pemba. Wanaoshughudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kushoto) na Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na benki hiyo kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...