Tabora Aprili 26, 2017, KATIKA kutimiza dhamira ya kutumia teknolojia
ya mawasiliano katika kuendeleza jamii, kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel kwa kushirikiana na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani
imeanzisha mpango utakaowawezesha wanafunzi wa sekondari kupata nyenzo
za masomo kupitia mtandao wao wa intaneti
Mafunzo hayo kwa kupitia mtandao yanayojulikana kama“Studi Academy”
yanapatikana kupitia mtandao wa Airtel wa 3G. ambapo katika kijiji cha
Mbola Mkoani Tabora Airtel kwa kushirikiana na Erickson wameboresha
zaidi mawasiliano ya intaneti ya kasi ya 3G ili kuhakikisha kuwa
shule na vituo vya huduma za afya zinafaidika na mpango huu kabambe
kwa kuinua upatikanaji wa huduma za masomo kupitia mtandao na kuanza
kuwafaidisha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu.
Akiongelea ujio na mafanikio ya mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya
sekodari ya Lolangulu , Cleophas Bugomba alisema” Shule yetu imekuwa
na changamoto ya walimu wa kutosha kwa masomo ya sayansi hivyo kuwepo
kwa masomo haya kupitia mtandao kumesaidia kupunguza changamoto hii
kwa kiasi kikubwa. Mafanikio haya tumeyaona kupitia matokeo ya
mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili ambapo ufaulu wa wanafunzi
hususani katika masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na fizikia umekuwa wa
kiwango kikubwa pamoja nakuwepo kwa changamoto hizi za walimu wa
kutosha wa masomo hayo”.
Kwa upande wake mwanafunzi wa kitado cha tatu mwaka 2017 Irene Tamson
ambayo pia ni mwanafunzi bora wa kike aliyefanya vizuri katika masomo
ya sayansi kwa mkoa wa Tabora alisema” mpango huu wa “Studi Academy”
unaowezeshwa na intaneti ya Airtel umenisaidia sana kufanya maswali
mbalimbali na kupata majibu sahihi hapo hapo, kujifunza vitu vipya na
kupata nyezo muhimu pindi nikijisomea binafsi au kwa makundi.
Tunafurahi kuweza kunganishwa na mtandao na kujifunza kutoka kwa
wengine kutoka nchi za ulaya lakini pia kupata nyenzo muhimu za
kujifunzia kwanjia ya technologia ya kisasa.”
Nae Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema,
“tunajisikia fahari kuwa na mtandao bora unaotuwezesha kutoa huduma
kwa jamii ikiwemo mpango huu wa Studi Academy, lengo letu Airtel ni
kutoa suluhisho kupitia teknolojia ya mtandao ili kuwafikia watanzania
wengi zaidi ili wapate mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kwa maeneo ya
pembezoni”.
Mipango na dhamira yetu Airtel ni kuendelea kushirikiana na wadau
wetu kama Ericsson na Health kutumia fursa ya mawasiliano kuiwezesha
jamii kwa kurahisisha baadhi ya changamoto za elimu na afya,”.
Alieleza Bi Bayumi
Airtel Tanzania pia kupitia mpango wake wa kuendelea kutoa mawasiliano
bora kwa kuzingatia ubunifu mwaka jana ( 2016) walishirikiana na VETA
na kuzindua Applikesheni kabambe ya VSOMO ili kuwawezesha watanzania
nchini kote kujisomea kozi za ufundi stadi kutoka kwenye vyuo vya
Ufundi VETA kupitia simu za mkononi ili kutoa fursa kwa watanzania
nchini kujiendeleza kielimu bila kujali changamoto zinazosababishwa na
mazingira au ukosefu wa vifaa vyakujisomea karibu nao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu iliyopo kijiji cha Mbola
mkoani Tabora wakisoma kwa kupitia njia ya mtandao baada ya Airtel kwa
kushirikiana na Erickson pamoja na taasisi ya Earth iliyoko nchini
Marekani kuwawezesha wanafunzi hao kupata nyenzo za masomo kupitia
mtandao kwa kupitia mpango ujulikanao kama “Studi Academy”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...