Mashamba ya mpunga ya Mbarali Highland Estates, Kapunga Rice Project, Kapunga Small Holders farm, pamoja na skimu za umwagiliaji za Mwanavala (Nguvukazi farm), Mwashikamile pamoja na Sikimu ya Mwendamtitu zilizoko Mbarali mkoa wa Mbeya yametozwa faini ya jumla ya kiasi cha shilingi 120,290,000/= baada ya kukiuka sheria mbalimbali za Mazingira zilizo chini ya Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe 27 aprili 2017, imetozwa na Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kuokoa Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilichoko Mkoani Mbeya kupitia kwa Mwananasheria wa NEMC- Vicent Haule , baada ya kugundua makosa mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za mazingira na umwagiliaji katika Mashamba hayo wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya Mpunga na skimu tofauti za umwagiliaji wilayani humo.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko cha Kitaifa Bwana Richard Muyungi, alisema kwamba kutokana na makosa mbalimbali yaliyokutwa katika masahamba hayo ikiwemo kutokuwa na vyeti vya ukaguzi wa Mazingira, kukiuka taratibu za umwagiliaji kwa kutoa na kutumia maji bila ruhusa, kuweka mifereji mikubwa ya kumwagilia mashambani pasipo kufuata sheria na kanuni zinazotakiwa, kutorekebisha miundombinu ya Umwagiliaji kwa mifereji ya kutolea maji. 
 

Mashamaba hayo yanapigwa faini kama ifuatavyo Mbarali Estates 33,000,000, Kapunga Rice Project 33,100,000/=, Kapunga Small Holders 3,000,000/=, Madibila farm Project 33,000,000. Pamoja na mashamba hayo pia zipo skimu za Umwagiliaji zilizotozwa faini ikiwepo Skimu ya Mwendamtitu 7,995,000, Mwanavala (Nguvukazi) 7,995,000/=, Mwashikamile 2,200,000/=.

Aidha aliongeza pia mashamba ya Mwashikamile, Mwanavala(nguvu kazi) na Kapunga Small Holders, wanatakiwa kulipa faini lakini pia baada ya kuvuna wanatakiwa kuacha mara moja kulima tena katika mashamba hayo mpaka pale watapofuata taratibu za kupata vibali vya maji na cheti cha ukaguzi wa mazingira kutoka NEMC na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji ."Kutoza faini hizi siyo kukomoa Mashamba haya ila ni kuhakikisha kuwa Wamiliki wa mashamaba makubwa ya umawagiliaji wote Nchini wanafuata taratibu na Sheria za kimazingira katika kuendesha mashamba haya" alisema Muyungi

Kikosi kazi hiko kiko MKoani Mbeya kwa kukagua na kutembelea sehemu mbalimbali za mashamba , skimu za umwagiliaji na pia kusikiliza maoni ya Wananchi jinsi ikiwa ni harakati za kurudisha ikolojia ya mto Ruaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...